MAAJABU YA DUNIA:BI. HARUSI ATOWEKA SIKU 4 KABLA YA NDOA

0 comments
Deogratius mongela
MTU mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Juma Mwinyivue maarufu kama ‘Tabambwa’ (28) mkazi wa Zogowale, Visiga mkoani Pwani, alijikuta katika wakati mgumu baada ya mwanamke aliyetaraji kumuoa, aliyetajwa kwa jina moja la Manka (20) kumzimia simu na kuingia mitini siku chache kabla ya ndoa yao, tukio lililotokea Mei 23, mwaka huu.
Juma Mwinyivue maarufu kama ‘Tabambwa' anayedaiwa kutorokwa na mchumbaake.
Kwa mujibu wa mpambe wa bwana harusi, Saidi Matakope, ndugu na marafiki wa bibi harusi walitayarisha ngoma maarufu ya Kigodoro na vyakula wakiamini binti yao atapata mume, lakini hadi ilipofika jioni, mwanaume hakuweza kutokea na kuwaacha watu vinywa wazi.
Katika eneo la tukio, mume mtarajiwa Juma, alisema alikutana na Manka na kumchumbia mwanzoni mwa Machi. Baada ya kuridhika na kukubaliana, ndoa ilipangwa kufanyika Mei 23, mwaka huu huku akiwa tayari ameshalipa mahari na kila kitu cha muhimu.
Lakini wiki mbili kabla ya ndoa, Juma alidai kutompata mke wake hewani baada ya kukubaliana kwenda kurekebisha shela la harusi, kitu kilichomshangaza kwani hata alipofika nyumbani kwake, alikuta mlango wa nyumba yake ukiwa umefungwa.
Juma alisema kuwa alipompigia simu yake ilikuwa haipatikani na kuamua kwenda kwa mama yake mzazi ambaye naye hakuwa akijua mwanaye ameelekea wapi huku siku zikiwa ukingoni.

Manka anayedaiwa kukimbia ndoa.
“Siku iliyofuata nikampigia mama yake akaniambia mwanaye ameelekea Iringa kwa shangazi yake. Nikashangaa na kuuliza kwa nini hakuniaga. Nilimpigia simu yake ikawa inaita, inakata au kutopatikana kabisa. Kwa hivyo nikamwambia mama mkwe kwamba mwanaye sitamuoa tena na nimesamehe gharama zote nilizotoa,” alisema Juma.
Mshenga wa Juma aliyejitambulisha kwa jina la Kindala, alidai baada ya kumtaarifu mama Manka kuwa ndoa hakuna, alishangaa baada ya wiki moja kupigiwa simu na ndugu zake aliulizwa muda ambao mwanaume angeenda kuoa.
“Ndipo tukashangaa na kuwaambia mbona tayari tumeshatoa taarifa kwa mama mtu kwamba hatuoi tena,” alisema mshenga huyo.
Kwa upande wake, bibi harusi alikiri kusafiri Iringa na shangazi yake, kwa kile alichodai ni kufanyiwa tambiko la ndoa, lakini akaogopa kumuaga mwenzake akijua wazi asingekubaliwa. “Bado nampenda na naitaka ndoa hata kesho nipo tayari, nilikwenda kwa shangazi Iringa siyo kwenye michepuko,” alisema Manka.

Read More »

AUNT LULU AJIBU HAYA KUFUATIA TUHUMA ZA KUWA NA VIRUSI VYA UKIMWI.

0 comments
                                                                         Aunty Lulu.
Makubwa! Kufuatia fununu kuwa mwanadada asiyeishiwa matukio mjini, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ ana ngoma na amejiunga kwenye kikundi cha watu waishio na virusi vya Ukimwi, mwenyewe amefunguka kwamba kama mtu ana uhakika ajitokeze waende pamoja wakapime.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda wikiendi iliyopita, Aunty Lulu alisema amekuwa akishutumiwa na watu kwamba ana ngoma jambo ambalo siyo kweli na mama yake ni shahidi kwani mapema mwaka huu walikwenda pamoja kupima na kukutwa yupo ‘biye’.
“Wanaonisema wanikome kabisa kwani hawana ushahidi na hawajawahi kunipima,” aling’aka Aunty Lulu.

Read More »

NINI KIMEIKUMBA NDOA YA MAIMARTHA?SOMA MKASA MZIMA HAPA.

0 comments
Mayasa Mariwata na Gladness Malya
Ooh…noo! Ile ndoa ya Mtangazaji Maimartha Jesse`Mai’ na mumewe, Raymond Shayo ‘Shaa’ inadaiwa kuwaka moto kufuatia ‘gogoro’ la ndani kwa ndani la mara kwa mara kwa wanandoa hao, kisa kikielezwa kwamba ni wivu uliokithiri wa mwanaume huyo.
Kwa mujibu wa mtu wa karibu na staa huyo, Shaa amefikia hatua ya kumkataza Mai kuhudhuria kwenye shughuli mbalimbali za mashosti zake na kujikuta akikaukiwa marafiki na kuishiwa ile shauku na utamu wa ndoa.
Alipotafutwa Mai na kusomewa ‘eituzedi’ ya sakata hilo alikuwa na haya ya kusema: “Nashindwa kulizungumzia si unajua mambo ya wanandoa ni siri? Ukweli mimi na mume wangu kuna kipindi huwa tunahitilafiana jambo ambalo ni kawaida katika ndoa,” alisema Mai.

Read More »

TAARIFA KUTOKA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

0 comments
Jana jumapili tarehe 24, Mei 2015 Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF imeketi katika ukumbi uliopo makao makuu ya Shirikisho uwanja wa Karume.
Kamati ya Utendaji imepitia masuala mbalimbali na kutoa maamuzi yafuatayo:
CLUB LICENCING (Leseni za vilabu)
Kamati ya Utendaji imeiagiza sekretarieti ivisisitize vilabu vya Ligi Kuu umuhimu wa kukamilisha maombi yao ya ushiriki wa ligi kuu kwa msimu wa 2015/16 kwa kuwasilisha fomu za maombi ya Leseni za vilabu TFF. Klabu ambayo haitakamilisha mchakato huo haitaruhusiwa kushiriki ligi kuu ifikapo msimu wa 2015/16.
KOMPYUTA - Kutokana na maamuzi ya mkutano mkuu wa TFF uliofanyika Morogoro ambao uliagiza wanachama wake wapya wapewe kompyuta, agizo hilo limetekelezwa na kompyuta hizo watakabidhiwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji wanaotoka kanda hizo ili waziwakilishe maeneo husika. Mikoa hiyo ni Geita, Katavi, Manyara, Njombe na Simiyu.
MFUKO WA FDF - Kufuatia mkutano mkuu wa TFF kuingiza kipengele cha FDF katika katiba yake, kikao cha Kamati ya Utendaji wa mujibu wa katiba kimepitisha kanuni za uendeshaji wa mfuko huo.

     Aidha kikao hicho kimeteua wajumbe wafuatao wawe wajumbe wa      tume hiyo

     (i)Tido Mhando - Mwenyekiti,

     (ii) Deogratius Lyatto - Makamu mwenyekiti

     (iii)Ephraim Mafuru - mjumbe,

     (iv)Beatrice Singano - mjumbe,

     (v)Joseph Kahama - mjumbe

     (vi)Ayoub Chamshana - mjumbe.

Pia Henry Tandau ameteuliwa kuwa katibu mtendaji wa mfuko huo.

AJIRA

Kamati ya Utendaji ya TFF imemteua Boniface Wambura kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Bodi ya Ligi Kuu nchini kuanzia tarehe 01, Juni 2015. Wambura kabla ya uteuzi huo alikua mkurugenzi wa mashandano  TFF.TFF inampongeza Wambura kwa uteuzi na inaamini atatoa mchango mzuri katika kukuza na kuzitangaza ligi zetu.

Kamati ya utendaji imemteau Martin Chacha (mratibu wa timu za Taifa) kukaimu nafasi ya mkurugenzi wa mashandano TFF.

TIMU ZA TAIFA

Kamati ya utendaji ya TFF imesikitishwa na mwenendo mbovu wa Taifa Stars Rais wa TFF, Jamal Malinzi kwa niaba ya kamati ya utendaji amewaomba radhi wapenzi wa mpira kwa matokeo mabaya ya Taifa Stars kwenye michuano ya  Cosafa.

Kikao cha kamati ya utendaji kilipokea taarifa juu ya mwenendo wa timu ya Taifa.Baada ya majadiliano ya kina, ilikubaliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa, Mart Nooij apewe changamoto maalumu ya kufuzu kwa fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN na asipofanikisha jambo hilo mkataba wake utasitishwa mara moja.

Maamuzi haya yamezingatia hali halisi ya timu ya Taifa ambayo inakabiliwa na michuano mbalimbali ya kimataifa ndani ya kipindi kifupi. Aidha katika kuliimarisha benchi la ufundi la timu ya Taifa, Leopald Tasso Mkebezi ameteuliwa kuwa meneja mpya wa timu ya Taifa.

Mkebezi amewahi kuwa meneja wa timu ya Taifa katika kipindi cha mwaka 2006 - 2012.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO

LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Read More »

MASKINI KAJALA APATA MATATIZO YA UBONGO

0 comments
Imelda mtema
Maskini Kajala! Ndivyo unavyoweza kusema ukisikia mkasa wa staa wa kiwango cha juu kwenye tasnia ya filamu za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’, ambaye anadaiwa kwa hivi sasa hayuko sawa kiafya baada ya kupigwa chupa kichwani akiwa katika shoo ya kumchangia mke wa msanii Mabeste iliyofanyika New Maisha Club, Masaki jijini Dar.
Kajala Masanja akionekana na jeraha usoni kipindi ambacho alikua amepigwa chupa.
TUJIUNGE NA CHANZO
Chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa Kajala kimeliambia Ijumaa Wikienda kwamba, tangu staa huyo akumbwe na sekeseke hilo amekuwa katika kipindi kigumu kwani amekuwa akipata maumivu makali sehemu ya kichwani huku akianguka mara kwa mara.
Kajala Masanja.
Kilidai kwamba, pia Kajala amekuwa akipata kizunguzungu kikali hivyo kujiona yupo kwenye hatari kubwa hasa ikitokea akaanguka vibaya kwani anaweza kupoteza maisha.
 ASHINDWA KUENDESHA GARI
Mpashaji wetu huyo aliweka wazi kuwa tangu Kajala akumbane na mkasa huo mzito uliomsababishia kushonwa nyuzi mbili juu ya jicho, amekuwa hayuko vizuri na kuna wakati hawezi hata kuendesha gari hivyo kukwamisha shughuli zake za kila siku.
“Kiukweli Kajala hayupo vizuri kabisa,  amekuwa kwenye kipindi kigumu mno tangu alipopigwa chupa klabu.
“Amekuwa akianguka mara kwa mara kutokana na kizunguzungu kikali anachopata akisimama au kutembea,” kilisema chanzo hicho.

 CT-SCAN;mfano wa mashine ambayo Kajala amefanyiwa vipimo.
ATINGA HOSPITALINI
Habari zilizidi kumiminika kuwa, baada ya kuona hivyo Kajala alikwenda kwenye Hospitali ya Regency iliyopo Upanga jijini Dar kwa ajili ya kufanya vipimo.
 AFANYIWA CT-SCAN
Kilisema kuwa alipofika hospitalini hapo alifanyiwa kipimo cha CT-SCAN kichwani ambapo majibu yalipotoka aliambiwa kuwa kinachomsumbua ni damu iliyoganda sehemu aliyopigwa chupa.
 MAJIBU YA DAKTARI
“Daktari alimpa majibu ya kushangaza maana alimwambia kama angezembea, tatizo lingekuwa kubwa sana kwenye ubongo na lingeleta shida zaidi,” kilisema chanzo hicho.
 HUYU HAPA KAJALA
Baada ya kunyetishiwa mkasa huo wa kusikitisha, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Kajala ili kuthibitisha tatizo hilo alilokuwa nalo ambapo alikiri kuwa alikuwa akihisi kizunguzungu kikali cha mara kwa mara lakini hakuwa amegundua kama alikuwa na tatizo la kuvilia damu kichwani.
“Lakini kwa sasa namshukuru Mungu niko sawa kidogo. Ukweli nilikuwa napata shida sana kila nikiinuka, napata shida ya kizunguzungu kikali sana,” alisema Kajala.
 TUJIKUMBUSHE TUKIO
Wakati Kajala akitoka Klabu ya New Maisha hivi karibuni, akiwa anashuka kwenye ngazi, ghafla alishangaa kurushiwa chupa kichwani iliyosababisha kuanguka kutoka kwenye ngazi hadi chini na kusaidiwa na wasamaria wema waliompeleka katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar ambapo alishonwa jeraha alilolipata.
Katika sakata hilo, Kajala alisema kuwa mtu aliyempiga chupa ni mwanaume na tayari yupo mikononi mwa polisi japo kabla ya tukio hilo alikuwa  hamjui na wala alikuwa hajawahi kumuona.

Read More »

MWIGULU NCHEMBA AJIUZULU NAFASI YA UNAIBU KATIBU MKUU CCM ILI KUWANIA URAIS

0 comments
Mwigulu Nchemba.
ALIYEKUWA Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwigulu Nchemba amejiuzulu nafasi hiyo ili awanie nafasi ya kugombea urais na nafasi yake imechukuliwa na Rajab Luhavi aliyekuwa mshauri wa rais katika siasa.
Mwigulu amabye pia ni Naibu Waziri wa Fedha, ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo leo jioni katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mkoani Dodoma.
Akithibitisha taarifa hiyo, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema kuwa Mwigulu ameamua kujiuzulu nafasi hiyo kutokana na nia yake ya kutaka kuomba kuwania urais kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
"Mwigulu alikuwa ameshamwambia nia hiyo Mwenyekiti wa Chama, Rais Jakaya Kikwete, naye akamkubalia, sasa leo katika kikao ameomba rasmi kujiuzulu na mwenyekiti amemkubalia mbele ya wajumbe wa NEC" Alisema Nape.
Nape amesema kufuatia uamuzi huo, Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete amemteua msaidizi wake katika masuala ya siasa, Ndugu Rajabu Ruhavi kuwa Mjumbe wa NEC, na wakati huohuo kumteua kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM kushika nafasi iliyoachwa na Mwigulu.

Read More »

AUNT EZEKIEL NA WEMA WAANGUA VILIO: NINI KIMEWASIBU SOMA MKASA MZIMA HAPA

0 comments
Imelda Mtema
Baada ya kula viapo vya kutozikana, wasanii wawili wa filamu Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Aunt Ezekiel Grayson wamejikuta wakiangua vilio wakati wakipatanishwa na rafiki yao mkubwa ambaye ni pedeshee anayejulikana kwa jina la Daudi Mambya.
Aunt Ezekiel akimbembeleza Wema baada ya kupatanishwa.
Habari kutoka kwa shuhuda wetu zilieleza kwamba, tukio hilo lilijiri wikiendi iliyopita kwenye Ufukwe wa Coco jijini Dar ambapo Daudi aliwaita kwa mwaliko wa mishikaki bila wenyewe kujua kinachoendelea.
Habari zilieleza kuwa, Daudi ambaye kwake huwa hawafurukuti, amekuwa akiumizwa mno na tofauti ya wasanii hao kwa sababu ni watu walikuwa wakipendana hivyo kugombana kwao kulikuwa kunaleta shida kwa marafiki zao wengine.
Imefahamika kwamba, Daudi alitumia ujanja wa kuzungumza na kila mmoja kwa wakati wake ambapo alibaini kuwa hakuna aliyekuwa tayari kupatana na mwenzake.
Ilisemekana kuwa, Daudi alitumia ujanja wa kitaalamu ili kila mmoja kumuweka sawa bila kujijua.
“Unajua Daudi ni rafiki yao sana, sasa hakuwa anapendezwa na tatizo ambalo limejitokeza hivyo alitumia njia tofauti ili kuweza kuwakutanisha pamoja tena waweze kupatana,” alieleza mtoa habari huyo.

Wakiwa na rafiki yao Daudi Mambya anayedaiwa kuwapatanishwa.
Ilielezwa kwamba Daudi alianza kwa kumtafuta Wema na kumpeleka Coco Beach akimuambia kuwa anataka akamnunulie mishikaki huku wakati huohuo akimwambia Aunt naye wakutane ufukweni hapo.Shushushu wetu alizidi kufunguka kuwa Daudi alitangulia Coco na Wema, huku akifanya mawasiliano na Aunt na baada ya muda, Aunt naye aliwasili huku kila mmoja akibaki katika mshangao usioelezeka baada ya kukutana uso kwa uso.
Sosi huyo alisema kuwa Wema na Aunt walipoonana kila mmoja alikuwa kimya lakini Daudi aliamua kuwasomea risala ndefu iliyomwingia kila mmoja.Mambo yakipokaa vizuri, wawili hao walishuhudiwa wakiwa wamekumbatiana huku kila mmoja akiangua kilio kilichochukua takribani nusu saa hivyo kufanya eneo hilo kuwa kama kuna msiba.
“Yaani mpaka Daudi mwenyewe alidondosha machozi baada ya Wema na Aunt kukumbatiana na kuanza kulia.
“Yaani ilikuwa simanzi kubwa sana,” alimalizia shuhuda huyo.Akizungumza na gazeti hili, Daudi alisema kuwa aliamua kuwapatanisha wawili hao kwa kuwa alikuwa hapendezwi na tatizo hilo na kwamba wote ni rafiki zake.
Kwa upande wake, Aunt alifunguka ya moyoni:
“Tulipokutana kila mtu alijua tatizo lake na tukaona ni mambo ya kijinga, ikabidi tuweke tofauti pembeni maisha yaendelee.”
Wema alisema: “Mambo ya kugombanagombana hayana msingi na kwa vile ni mtu mzima (Daudi) aliwakutanisha, nikaona yaishe.”Wema na Aunt ambao walikuwa marafiki wakubwa waliingia kwenye mgogoro hivi karibuni baada ya Wema kumtuhumu Aunt kuunga mkono shoo ya Zari All White Party ya mwanadada Zari Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ambaye ni mpenzi wa aliyekuwa mpenzi wa Wema, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Read More »

DIAMOND 'AMAZING' SHOO YAKE ALIYOFANYA LONDON YAACHA GUMZO

0 comments
Musa Mateja
AMAZING! Hiyo ndiyo kauli pekee unayoweza kuitamka kuakisi shoo baab’kubwa aliyoifanya mkali wa wimbo wa Nasema Nao, Nasibu Abdul ‘Diamond’, London, Uingereza, Risasi Mchanganyiko linakujuza zaidi.
Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ akipagawisha wakazi wa jiji la London.
Shoo hiyo iliyoacha gumzo la aina yake nchini humo kutokana na kupata idadi kubwa ya mashabiki, ilifanyika Jumapili iliyopita katika Ukumbi wa Royal Regency, maeneo ya Manor Park.
Chanzo chetu kilichoambatana na msafara wa Diamond kwenye shoo hiyo ijulikanayo kama Diamond are Forever, kiliweka bayana kuwa shoo hiyo ilikuwa ya kustaajabisha (amazing) kwani ilikadiriwa kuwa na watu zaidi ya 1500 ambao ni Wabongo waishio nchini humo waliochanganyika na wazungu.

Akitambulishwa mbele ya mashabiki.
“Jamaa kapiga shoo ya nguvu, watu walijaa kweli, si Wabongo pekee bali Wazungu nao walikuwepo. Si zile shoo za kupiga sebuleni ambazo wasanii wengi wa Kibongo huwa wanafanya. Yani hadi leo (Jumatatu) kila mtu anaizungumzia. Imeacha gumzo la aina yake.
“Ilikuwa yenye hadhi maana kiingilio kilikuwa ni shilingi laki moja na ishirini kwa V.I.P na elfu tisini viti vya kawaida, Wazungu walichanganyikiwa hadi ikabidi waulize Who is Diamond? (Diamond ni nani?) wakaambiwa na meneja wa msanii huyo, Babu Tale kuwa ni msanii anayeiwakilisha Tanzania akitokea Tandale, Dar es Salaam,” kilimwaga data chanzo hicho.
Mbali na umati huo ‘kuinjoi’ nyimbo za Diamond kama Kamwambie, Mbagala, Kesho na Nasema Nao na nyingine kibao, shoo hiyo iliongeza msisimko kufuatia uwepo wa balozi wa Tanzania nchini humo, Mhe. Peter Kalaghe ambaye alipewa nafasi ya kuzungumza machache jukwaani, burudani ikaendelea.

Read More »

Baada ya Kupotea kwa Muda: Wema Sepetu Arudi tena Kuigiza Akiwa na JB- VIDEO

0 comments
Staa mrembo wa Bongo Movies, Wema Sepetu ameshare nasi video ya kazi mpya  inayokwenda kwa jina la  Chungu Cha Tatuakiwa na Staa mwnzake, Jacob Stephen  'JB'.


Kwa muda mrefu sasa Wema Sepetu amekuwa afanyi filamu, Bila shaka mashabiki wake wana hamu kubwa sana ya kumuona tena kwenye filamu.
Jionee kipande cha kazi hiyo  HAPA

Read More »

NEW AUDIO: NAY WAMITEGO Ft. DIAMOND PLATNUMZ – MAPENZI au PESA

0 comments
Kusikiliza na kudownload wimbo huu, click hapo chini.
https://soundcloud.com/nicolaus-trac/nay-wamitego-ft-diamond-platnumz-mapenzi-au-pesa

Read More »